Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Thursday, August 19, 2010

POMBE SI CHAI YA MAZIWA!!!!


Mwanamke na mwanaume mmoja, mwishoni mwa wiki iliyopita 'walikata network' na lijikuta wakilala barabarani usiku kucha,baada ya kudaiwa kufakamia pombe za kienyeji katika klabu ya pombe hizo maeneo ya Mji Mpya mkoani hapa.

Watu hao ambao haijafahamika mara moja kama ni mke na mume,walikutwa na mwandishi wetu,jirani kabisa na kilabu hicho cha pombe za kienyeji wakiwa 'wamenoki' kwa kupoteza mawasiliano kiasi cha kudhaniwa wamekufa.

Daadhi ya majirani wanaoishi katika eneo hilo waliueleza mtandao huu kwamba jamaa walilala hapo usiku kucha, ambapo imedaiwa walizinduka saa mbili asubuhi baada ya kumwagiwa maji ya baridi na wasamaria wema! Pombe si......

No comments:

Post a Comment