Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Thursday, August 26, 2010

SKENDO


The Talented Cute wa Kiwanda cha Filamu Bongo, Jacqueline Wolper anatengeneza kichwa cha habari kwa mara nyingine na safari hii anasimulia jinsi alivyokoswa-koswa kwenye jaribio la kubakwa na mjomba wake anayeitwa Axaud Macha.

The 5star Paper, Risasi Mchanganyiko lina kisa kamili baada ya kufanya mahojiano na Jacqueline, wiki iliyopita, jijini Dar ambapo pamoja yote aliyosimulia, alisema kuwa lilikuwa ni tukio ambalo anamshukuru Mungu kwamba aliponea chupuchupu.

Alisema, alinusurika kubakwa Jumatatu ya Agosti 16, 2010 nyumbani kwake, Chentemba, Kinondoni, Dar na tukio hilo lipo Kituo cha Polisi Oysterbay likiwa limenakiliwa kwenye kitabu cha Ripoti za Rolisi (Report Book “RB”) nambari OB/RB/14500/2010.

Akisimulia tukio hilo kwa ‘paparazi’ wetu, Jacqueline alisema kuwa alikuwa anamheshimu mjomba wake ndiyo maana hakusita kumkaribisha nyumbani kwake, lakini alichomfanyia kimemfanya amtoe thamani.

Alisema, ni Mungu tu ndiye aliyemsaidia kupona katika jaribio hilo la kubakwa kwasababu mjomba wake alikuwa amekwishamvua nguo za juu na kubakiwa na brazia a.k.a sidiria.

“Jamani nyie waoneni hivi wajomba, kumbe wakati mwingine wana yao kutaka kuonja watoto wa dada zao, huyo mjomba wangu nimemtoa thamani,” alisema Jacqueline.

Akisimulia ‘in&out’, Jacqueline alisema, alianza kuwa karibu na mjomba wake alipotaka kununua gari.“Nilikuwa na shilingi milioni tatu, nikamuomba mjomba anikopeshe shilingi milioni nne akanikubalia, kwahiyo nikanunua gari aina Crester lenye namba za usajili T704 BBL.

“Nikiwa sijui hili wala lile, mjomba akaenda kuzungumza na polisi wakanikamata eti gari langu ni la wizi na mpaka sasa lipo polisi.

“Siku hiyo akaja nyumbani kwangu, tukiwa wawili tunazungumza, ghafla alinigeuzia kibao na kutaka kunibaka. Akanivua nguo na kuanza kunipiga picha za utupu. Alipotaka kunivua nguo zote nikapiga kelele akakimbia,” alisema Jacqueline.

Akaendelea: “Baada ya hapo amekuwa akitembea huku na huko ili kunichafua na anatishia kuzitoa picha ambazo alinipiga siku hiyo magazetini ili kunichafua.”

Baada ya kupata ishu hiyo, gazeti hili ‘lilimvutia waya’, Macha ambaye alisema kuwa Jacqueline anataka kupotosha ukweli kwa sababu ni demu wake wa muda mrefu.

Alisema, hata gari ambalo Jacqueline anadai ni lake si kweli na kwamba hilo ni mali yake.
“Nilimpa gari na nikampangia nyumba. Yule siyo mtoto wa dada yangu, ni demu wangu. Nilikwenda Magomeni Polisi kutoa taarifa baada ya kuona amekaa nalo muda mrefu bila kurudisha,” alisema Macha na kuongeza:

“Gari nilimuazima na sikumpa, kwahiyo nilipoona harudishi kwanza nikwenda Kijitonyama ambako nilikuwa nimempangia, nikaambiwa amehama. Nikaambiwa yupo Magomeni ambako nako niliambiwa amehama, nikawa sina jinsi nikaenda Polisi Magomeni.
“Polisi aliitwa, alipoulizwa akasema gari ni lake, akaambiwa aoneshe vielelezo vya kumiliki gari akakosa.”

Katika maelezo ya Macha, alisema kuwa baadaye msanii wa maigizo, Rashid Nassor ‘Chiddy’ alikwenda Polisi Magomeni na kujieleza yeye ndiye mmiliki wa gari hilo na alimuazima Jacqueline lakini alipoombwa nyaraka zinazomuonesha yeye ndiye mwenye mali, alikosa.

Gazeti hili, linaendelea kulifanyia kazi sakata hilo na linaahidi kwamba mwisho wa siku litamaliza huu mpira ambao wahusika wanatupiana.

1 comment:

  1. Jodi Jill could be described as covering the matter LIVE from
    Television. Rrt's going to by no translates to modify currently clearly one of essentially the most common purses at any moment. Its own top dog search queries of 12.100 likewise very much not up to America's.
    http://eve.sapporoplus.com/WebBoard/data/7/page_7_67.
    html

    ReplyDelete