Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Monday, August 16, 2010

Utafiti global publishers!


Mwandishi Wetu na Mashirika ya Habari
Utafiti wa kisayansi uliofanywa hivi karibuni nchini Marekani na Uingereza kisha kuripotiwa na Jarida la New Study umebainisha kwamba, wanawake wenye matiti makubwa huwasisimua zaidi wanaume kimapenzi kuliko wengine.

Jane Pincott Mwandishi wa masuala ya sayansi amekiri katika kitabu chake cha ‘Do Gentleman Really Prefer Brondes’ kwa kueleza kinagaubaga juu ya utafiti huo kuwa , nguvu ya mvuto wa wanawake wa aina hiyo ni kubwa na kufafanua kwamba ina uwezo mara dufu wa kuteka hisia za wanaume.

“Hakuna mwenye kupinga kuhusu hili, dunia nzima inafahamu na hasa wanaume wenyewe…kigezo cha kwanza cha kumtambua mwanamke ni matiti, …kadiri yanavyokuwa makubwa utambulisho wake hukua na mvuto huongezeka.

“Mwanamke kuwa na sura nzuri peke yake haitoshi…ingawa wanaume hupenda hilo pia, lakini si jambo linaloamsha hisia zao za mapenzi haraka, tumetafiti na kubaini ukweli huu tunaoueleza,” alisema Pincott alipozungumza na New Study.

Timu ya wataalamu iliyoendesha utafiti huo, ilihusisha zaidi ya wanaume 4,000, kwa kuwaweka kwenye chumba chenye picha za wanawake wenye matiti makubwa na madogo, ambapo ilibainika asilimia 79 ya waliotazama picha za wanawake wenye matiti makubwa walisisimka kimapenzi.

Naye Dk. Grazyna Jasienska wa Chuo cha Harvard aliongezea nyama kwenye uchunguzi huo kwa kusema kuwa, mwanamke mwenye matiti makubwa ana uwezo wa kushika ujauzito haraka kuliko aliyenayo madogo.

Ripoti hiyo ya watafiti wa nje inaweza kuwa na ukweli hata kwa wanawake wa kibongo ambao nyakati hizi wamekuwa wakiacha nje sehemu kubwa ya matiti yao makubwa, bila kubainisha sababu wazi za kufanya hivyo.

“Nakubaliana kwa kiasi fulani na utafiti huo kwa sababu za kitaalamu, matiti ni kiungo nyeti chenye hisia za mapenzi, kinapoonekana kwa wazi huvutia, hii haijalishi kama ni matiti ni makubwa au madogo.

“Lakini kwa kuwa matiti makubwa huonekana kirahisi mwanamke anapokuwa amevaa nguo, hiyo inaweza kuwa sababu ya wenye matiti hayo kuvutia,” alisema Richard Manyota mwanasaikolojia mahiri nchini.

Warembo wa kibongo wenye matiti makubwa ambao wamekuwa na tabia ya kuyaweka wazi bila kueleza kama wanatumikia utafiti huu ama la ni pamoja na Aisha Ramadhani ‘Isha Mashauzi’ (pichani), Aunt Ezekiel, Moureen Gislary, Ndumbagwe Misayo ‘Thea’, Fideline Iranga, Rehema Chalamila ‘Ray C’ na wengineo.

2 comments: