Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Friday, August 20, 2010

Msiba Algeria


Uongozi wa jumuiya ya wanafunzi wa kitanzania wanaosoma nchini Algeria (ATSA), wanasikitika kutoa taarifa ya kifo cha mwanafunzi mwenzao ndugu Felix Matela, kilichotokea siku ya tarehe 05/08/2010 Jijini Algiers nchini Algeria.

Ndugu Felix alikuwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Houari Boumediene (USTHB) Kilichopo jijini Algiers , Algeria . Alikuwa akiishi katika Hostel za chuo zinazotambulika kwa jina la CUB 3.

Uongozi unatoa shukrani za dhati kwa wizara ya elimu na ufundi na ubalozi wa Tanzania-Paris, Ufaransa kwa ushirikiano wao mkubwa katika kuhakikisha usafirishaji wa mwili wa marehemu kurudishwa nyumbani unakamilika pia uongozi unatoa shukrani kwa serikali ya Algeria kwa kujitolea kusafirisha mwili wa marehemu mpaka Tanzania.

Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa hivi karibuni mara tu taratibu za kusafirisha mwili wa marehemu zitakapo kamilika.

Tunawasihi familia, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu.

Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehem.

Uongozi – ATSA.
00213551713920,
00213553271791
tz_students@yahoo.fr

No comments:

Post a Comment