Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Thursday, August 19, 2010

Neno La Leo: Kuvua Au Kutokuvua? Ni Swali La Kizushi!


Jana jioni jamaa mmoja wa Idara ya intelijensia ( Tanzania) aliniuliza swali la ‘ kizushi’ ; “E bwana nataka kuifahamu Jiografia ya hapa, hivi wewe unakaa nyumba ‘A’ au’ B’? ” Aliniuliza. Jamaa huyu amekaa mahali hapo kwa miaka 20. Anafahamu kuwa nakaa nyumba ‘ B’ na kuna siku alinitambia kwa kuniambia alichosikia kwenye mazungumzo yangu ya simu wakati akipita nje ya nyumba ‘ B’ ninayoishi, yalikuwa mazungumzo ya kawaida tu. Iweje leo aniulize swali hili? Nilijiuliza. Kila swali lina tafsiri yake. Usikimbilie kujibu swali kabla hujalitafsiri. Jamaa yangu huyu alitakla kujua kati ya mawili yafuatayo; Mosi, kama nitajibu nakaa nyumba ‘ B’ nitamwambia nani anakaa nyumba ‘ A’. Huenda kuna mtu ameingia nyumba ‘ A’ lakini hajamjua ni nani. Pili; anamfahamu anayekaa nyumba ‘ A’ lakini anataka kujua kama namfahamu jirani yangu huyo. Jibu langu likawa; ” Mimi nakaa nyumba ‘ B’ na bila shaka unafamhamu anayekaa nyumba ‘ A’ , ni fulani. Hilo la mwisho nilimaanisha pia kuwa alimfahamu anayekaa nyumba ‘ B’. Naam. Kuvua au Kutokuvua, ni swali la kizushi. Na hasa kama anayeuliza swali tayari ameshashika mshipi na ndoano yenye chambo! Na hilo ni neno la leo.

No comments:

Post a Comment