Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Tuesday, September 7, 2010

Edward Nino: Mcolombia, mtu mfupi zaidi duniani


Edward Nino Hernandez akiwa na nakala ya kitabu cha kumbukumbu cha Guinness (Guinness World Record Book) baada ya kudai kushikilia rekodi ya mtu mfupi zaidi duniani.

REKODI ya mtu mfupi zaidi duniani inadaiwa kushikiliwa na Edward Nino (24), raia wa Colombia, ambaye ana urefu wa sentimita 70 au inchi 27.

Nino ametambuliwa rasmi na Rekodi za Dunia za Guinness kuwa ni mtu mfupi zaidi duniani baada ya mtu aliyekuwa akishikilia rekodi hiyo, He Pingping, raia wa China, ambaye alifariki mwezi Machi mwaka huu akiwa na urefu wa inchi 22.

Nino, mwenye uzito wa kilo 10 anajifunza kucheza sinema akiigiza kama jambazi “dogo” lenye kuuza madawa ya kulevya lakini likauawa katika mashambulio ya bunduki.

Nino, anayesema anapenda kucheza dansi, hapo nyuma alikuwa akinengua katika baa moja.





Akionyesha umahiri wake katika kucheza dansi huko Bogota ambako anafanya kazi kama kibarua.

Wazazi wake wanasema kaka wa Nino pia ni mfupi, akiwa na inchi 37 tu, lakini kaka zake wengine watatu wana vimo vya kawaida. Wazazi hao walimpoteza binti yao ambaye naye alikuwa na ufupi kama huo mnamo 1992, akiwa bado hajatimiza hata mwaka mmoja tangu azaliwe.

Nino anayetoka eneo la Bosa katika wilaya maskini ya Bogota, ana afya njema japokuwa huwa analalamikia kutoona vizuri. Pia ana rafiki wa kike mwenye umri wa miaka 18 aitwaye Fanny ambaye ana urefu wa futi tano, ambao ni urefu mkubwa sana ukilinganishwa na yeye.

Anasema huwa anajisikia vizuri tu kuhusiana na urefu wake, japokuwa anasema watu saa nyingine humkera kwa kumshikashika.


Akisuburi usafiri nyumbani kwake kwenda kazini.

Matumaini yake ni kutaka amiliki gari aina ya Mercedes (Benz) na kukutana na watu mashuhuri kama Jackie Chan, Sylvester Stallone na rais wa zamani wa Colombia, Alvaro Uribe.

Hata hivyo, rekodi yake hiyo inaweza kuvunjwa karibuni na Khagendra Thapa Magar wa Nepal ambaye ana aurefu wa sentimita 56, akiwa ni kijana mfupi zaidi duniani hadi atakapotimiza miaka 18 Oktoba 14 mwaka huu

No comments:

Post a Comment