Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Sunday, September 19, 2010

KIBAKA AKIONA CHA MOTO, AIVISHWA AKIWA ANAJIONA!


KIBAKA mmoja ambaye hajafahamika jina lake wala makazi ameuawa kikatili na wananchi wenye hasira kali na kisha kuchomwa moto baada ya kufanya jaribio la kuvunja duka na kuiba bidhaa mbalimbali. Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia juzi majira ya saa 10 alfajiri katika eneo la Mwenge Manispaa ya singida ambapo kibaka huyo alikuwa na wenzake watano. Kwa mujibu wa watu walioshuuhudia tukio hilo walisema kuwa vibaka hao wakiwa watano waliingia katika duka moja la Daniel Miyanji na kuanza kuvunja mageti ya duka hilo kisha kutoa bidhaa mbalimbali zikiwemo bia.

Mdogo wa mmiliki wa duka hilo Daniel Miyanji alisema akiwa amelala usiku huo alisikia kelelele za mbwa wa jirani wakibweka mfululizo. "Baada ya kusikia kelele za mbwa wa jirani muda mrefu niliamka na kuchungulia dirishani na kuona watu wakitoa vitu dukani kwetu, ndipo nilimwamsha kaka yangu na watu wengine juu ya tukio hilo." alisema.

Miyanji alisema kuwa hapo ndipo waliungana na kuanza kuwakurupua vibaka hao ambapo katika kurupushani hizo walifanikiwa kumkamata kibaka aliyekuwa ndani ya duka akitoa mali kwa wenzake na kuanza kushambuliana. Alisema kuwa kibaka huyo alikuwa akiwatisha kwa kisu lakini kutokana na umoja wa wananchi waliofika kutoa msaada baada ya kupiga makelele walimzidi nguvu na hatimae kuanza kumshambulia.

No comments:

Post a Comment