Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Sunday, September 19, 2010

WANANCHI WANGU KUNYWENI POMBE NA MVUTE SIGARA KWA WINGI, ASEMA WAZIRI WA URUSI


Nchi ya urusi ni miongoni mwanchi zinazoongoza duniani kwa unywaji pombe. Na sasa Waziri wa fedha wa nchi hiyo ametoa kali baada ya kuwataka wananchi kunywa pombe kwa wingi na kuvuta sigara zaidi ili kusaidia kukuza uchumi wa nchi hiyo.

Ingawa mara nyingi wanasiasa huwataka wananchi kuzingatia afya bora, bwana Kurdin amewataka wananchi wake kupiga tungi na kuvuta sigara zaidi ili mapato ya taifa yaongezeke. “Ukivuta pakiti moja ya sigara, inamaanisha unasaidia kutatua matatizo ya kijamii” amesema waziri Kurdin. “Watu lazima waelewe, wale wanaokunywa na wavutaji, wanasaidia sana kujenga nchi”.

Hii ni kali, labda wakati anaongea haya, na yeye alikuwa ameshapombeka kidogo.

No comments:

Post a Comment