Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Sunday, September 19, 2010

MATRAFKI WAPENDAO RUSHWA WAPIGWA CHENGA KWA MTANDAO


Hii imetokea huko nchini south Africa ambapo jeshi la polisi limetishia kumkamata na kumshitaki mtu anaetumia mitandao ya twitter na facebook kuwaonya waendesha magari au kuwapa tarifa zihusianazo na mahali walipo matrafiki. Baadhi ya watu huzikwepa barabara hizo na kuwaacha wapenda rushwa hao wakiwa wanakodoa macho kwa kukosa kitu kidogo kutoka kwa madereva.

Jamaa huyo kupitia mitandao hiyo anajiita “PIGSPOTTER”na anafanya hivyo kwa lengo la kupigana na rushwa iliyokithiri katika barabara za nchi hiyo. Akiwa anatumia simu aina ya blackberry anawataarifu waendesha magari na watumiaji wa mitandao hiyo maeneo mbalimbali yanayokuwa na mapolisi.

Katika kukubalika kwa kazi anayoifanya wananchi wametokea kumtetea, na yeye anasema anawaheshimu sana mapolice wanaofanya kazi zao vizuri lakini kwa wale walarushwa wasahau kuipata heshima yake.

No comments:

Post a Comment