Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Thursday, September 23, 2010

Neno La Leo: Degedege Si Ugonjwa Wa Watoto Tu


Na Maggid Mjengwa,
KWA kawaida degedege ni ugonjwa wa watoto. Dalili zake ni mtoto kupandwa na homa na mwili kutetemeka . Ni ugonjwa wa hatari sana. Utotoni tuliamini, kuwa ukiugua degedege, basi, hutaugua tena ukubwani.

Kumbe, kuna degedege la ukubwani pia, hususan kwenye masuala ya siasa na kampeni za uchaguzi kama hizi za sasa. Nilipata kuandika, kuwa siku hizi kila asubuhi ni burudani kusoma baadhi ya vichwa vya habari magazetini au kuangalia habari za kwenye runinga na kusikiliza redio. Kila kukicha kuna kituko kipya Afrika, ilipatwa kusemwa

No comments:

Post a Comment