Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Tuesday, September 7, 2010

POLE SANA MR NICEJana mwenye nyumba wa Mr Nice alimpigia simu Gea Habib aende akamsikilize Nice maana kuna matatizo yanayomkabili.Basi Gea akaenda huko Mwananyamala kwa manjunju na mama mwenye nyumba kumuita Nice wakakaa kuzungumza...Gea anasema Mr.Nice alikuja akichechemea akitokea chumbani.

Nice akaeleza kuwa juzi kulitokea ogomvi kati ya mpenzi wake na ndugu zake yeye akiwa ndani anawasikiliza na katika ugomvi huo ndugu walikuwa wakimtuhumu mpenzi wa Nice kuwa siku hizi anawabagua kisa yupo na Nice.Nice aliposikia jina lake likitajwa akatoka nje akawaambia ndugu hao waache kutaja jina lake yaani wasimuhusishe katika ugomvi wao.Baadae ugomvi huo ukaisha na kila mmoja kutawanyika.


Ilipofika usiku saa tatu ikaja gari na wakaka wawili na mmoja wa ndugu wa yule mpenzi wa Nice anaitwa Zulfa wakamuita Nice wakajitambulisha wao ni police na wamepokea malalamiko kutoka kwa huyo dada kuwa kampiga na wamekuja kumkamata.


Wakamuonyesha RB ya yule dada na Nice akaamriwa atoke ili aende kituoni kulikopelekwa malalamiko.Nice hakubisha akaondoka nao kwenye gari yao ndani ya gari wakamwambia wao sio polisi wala nini ila watamkomesha basi wakamfunga kitambaa usoni,wakampiga sana na kumsababishia majeraha.

Baaada ya kipigo wakamuita jamaa yao mwingine aje na kamera anasema wakamvua nguo na kumpiga picha akiwa mtupu..wakamfungua kile kitambaa walichomfunga usoni wakamlazimisha aiangalie kamera wakampiga picha nyingi sana.


Wale watu wakamwambia una bahati una Ukimwi la sivyo tungekufanyia mambo makubwa zaidi ya hayo.Na wakati wanampiga wakawa wanaambiana msimtoe damu maana mkimgusa mtaambukizwa Ukimwi.

Nice akaendelea kuelezea kuwa toka saa tatu usiku walipomchukua mpaka saa nane ndio wamekuja kumtupa uwanjani Temeke huko akiwa mtupu na nguo wakamtupia pembeni. Walipoondoka ndio na yeye kutoa kitambaa machoni akavaa nguo zake na kuomba msaada wa usafiri wa tax maana hakuwa na hela wala simu.

Nice akarudi mwananyamala na kwenda kutoa taarifa polisi na polisi jana wakafanikiwa kumkamata huyo dada ili aeleze wale watu ni kina nani na kwa nini wamefanya vile.Nice alilia sana na akasema hajapendezwa na kitendo alichofanyiwa kwani kinamuuma na kummsononesha sana
Jamani mie sielewi Mr.Nice amekuwa akiandamwa na zimwi la kupigwa pigwa kila siku sijui kwa nini

No comments:

Post a Comment