Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Thursday, June 3, 2010

AL GORE KUTENGANA NA MKE WAKE BAADA YA MIAKA 40!


Aliyekuwa Makamu wa Rais wa Marekani,Al Gore,ametangaza kutengana na mke wake, Mary Elizabeth “Tipper” Gore, baada ya miaka 40 ya ndoa!

Kwa mujibu wa barua pepe waliyowatumia marafiki zao na baadaye kuthibitishwa na msemaji mkuu wa Al-Gore.

Wanandoa hao ambao wiki kama mbili zilizopita walisheherekea miaka 40 ya ndoa yao,kwa pamoja wamesema wamefikia uamuzi wa kuifikisha mwisho ndoa yao baada ya mlolongo mrefu wa majadiliano baina yao.Hawakutoa maelezo zaidi na wameomba watu wote kuheshimu maamuzi na faragha yao.

Al Gore, mshindi wa Tuzo ya Nobel,ambaye watu wengi wanaamini alipokonywa ushindi wa kiti cha urais na George W.Bush mwaka 2000, alikutana na mkewe tangu wakiwa shule ya sekondari. Walioana tarehe 19,Mei mwaka 1970 huko Washington,DC. Wana watoto wanne wakubwa.

Ama kweli aliyesema kwamba ndoa sio mchezo wa kuigiza bila shaka alikuwa na mantiki.

1 comment:

  1. Acha kukopi na kupaste tu habari za watu.Keti chini andika.Hii umekopi pale bongocelebrity.Ntawaambia wenyewe

    ReplyDelete