Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Saturday, June 12, 2010

Wanawake wasomi CCM, Upinzani akuu!! Oyee!!


Wapinzani walalamikia wanawake wasomi kujiunga CCM.

Viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani wamelalamika kuwa wanawake wasomi hawataki kujiunga na vyama vyao badala yake wanakimbilia kujiunga kwenye Chama Cha Mapinduzi.

Hali hiyo inavifanya vyama hivyo kukosa wagombea makini na wasomi wa kuwasimamisha kugombea ubunge kwenye majimbo mbalimbali.

Wanasiasa hao wanalalamika kuwa wanawake wasomi wanaona ni kupoteza muda kufanya siasa katika vyama hivyo na kwamba ndio maana wanakimbilia CCM na wale ambao hawana mapenzi kwa chama hicho tawala wanaona njia pekee ni kujiunga kwenye asasi za kiraia.

Baadhi ya viongozi wa vyama hivyo waliohudhuria warsha ya kuhamasisha viongozi wa vyama vya siasa kuhusu mambo ya jinsia na uchaguzi, walisema wanawake wengi wasomi ambao wana mwelekeo wa kufanya siasa wanapenda kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Wanasiasa hao walisema wanawake wanapenda kujiunga kwenye chama hicho kwa vile wanaona huko hakuna kazi ngumu ya kufanya siasa kuliko ilivyo kwa vyama vichanga ambavyo bado vinafanya kazi ya kujiimarisha ili viweze kupata wafuasi wengi.

Warsha hiyo madhumuni yake yalikuwa ni kujadili namna vyama vya siasa vitakavyofungua milango kwa wanawake kujitokeza kugombea ili kutimiza lengo la kuhakikisha uwakilishi kwenye bunge unakuwa asilimia 50 kwa 50.

Mwenyekiti wa NLD Dk Emmanuel Makaidi alitoa mfano wa Anna Senkoro ambaye alijitokeza kugombea urais kwa tiketi ya PPT Maendeleo kuwa alilazimika kukihama chama hicho na kujiunga CCM baada ya kubaini kuwa kwenye vyama vya upinzani ni lazima atoe fedha yake kuendesha shughuli za chama.

“Huyu alilalamika kuwa wakati anaumwa hakupata msaada kutoka kwa chama chake, ila kwa vile Rais Jakaya Kikwete alimsaidia wakati anaumwa akaona ni bora amfuate huko…zile shida za kukosa usingizi kufikiria utapata wapi fedha wanawake hawataki hayo,” alisema Dk. Makaidi.

No comments:

Post a Comment