Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Wednesday, June 2, 2010

Israel yakemewa kwa kushambulia meli za Gaza!Serikali ya Uturuki imelaani Israel katika mkutano wa dharura wa baraza la usalama la umoja wa mataifa kwa kushambulia meli zilizokuwa zinapeleka chakula cha msaada katika ukanda wa Gaza hapo jana.

Takriban wanaharakati tisa wa Palestina waliuawa baadhi wakiwa raia wa Uturuki, wakati Israel ilipovamia meli hizo zikiwa baharini.

Kwa mujibu wa waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Ahmet Davutoglu, serikali ya Israel imefanya mauaji na ameitaka iombe radhi kwa kosa hilo, kuwachia meli hizo na kuwalipa fidia wanaharakati wa kipalestina.

Waakilishi wa Israel kwenye mkutano huo wamesema kuwa hatua ya wanajeshi wao ilikuwa ya kujilinda kutokana na tisho la uvamizi.

Wakati huo huo, waziri wa ulinzi wa Israel, Ehud Barack,ameelezea alitumai jamii ya kimataifa ingeelewa tisho la usalama inalokabiliwa nalo kutoka kwa kundi la wapiganaji la hamas.

No comments:

Post a Comment