Habari mbalimbali toka pande za bongo bila kusahau matukio mbalimbali yanayorindima pande zote za dunia
Psquare Ft. J.Martins- E No Easy
Thursday, June 3, 2010
Zimbabwe yachapwa na Brazil 3-0 nyumbani kwao!
Mchezo wa kirafiki wa kimataifa kati ya Brazil na Zimbabwe, umemalizika hivi punde, huku Brazil ikiibu kidedea kwa kuwachakaza Zimbabwe kwa mabao matatu kwa bila, 3-0.
Mchezo huo ulianza kwa Zimbabwe kushambulia lango la Brazil na kufika langoni mara kadhaa huku washambuliaji wa Zimbabwe wakiwa na mcheche kila walipolifikia lango la Brazi na kupiga nje kiasi cha kukosa magoli 2 ya wazi katika kipindi hicho cha kwanza.
Mchezo ulibadika ambapo Brazil walianza kuandika mabao katika dakika ya 42 kipindi hicho cha kwanza kupiti mchezaji wao mahiri, Bastus, aliyefunga kupitia mpira wa adhabu ndogo alioupiga na kuvuka ukuta na hatimaye kutinga moja kwa moja wavuni.
Robihno naye aliiandikia bao la pili kwa timu yake katika dakika ya 44, baada ya kuwatoka mabeki wa Zimbabwe na kuachia shuti kali lililomwacha kipa hoi na kutinga wavuni.
Hadi timu hizo zinakwenda mapumziko, Brazil ilikuwa ikiongoza kwa mabao 2-0, na kipindi cha pili Elano, aliipatia timu yake ya Brazil bao la tatu (3) na la ushindi, kufuatia pasi nzuri na kufanya mchezo huo kumalizika Brazil ikiwa mbele kwa mabao 3-0.
Taifa Stars tukae chonjo tusiwe na mcheche kama waliokuwanao zimbabwe kwani katika kipindi cha kwanza walikuwa na kila hali ya kufunga magoli lakini sijui kilichowasibu, kazi kwetu Wabongo siku hiyo ya jumatatu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment