Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Friday, June 4, 2010

MAHARAMIA SASA KUHUKUMIWA NCHINI!!!



Serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania chini ya rais wake Mh.Jakaya Mrisho Kikwete imetoa tamko la marekebisho ya kifungu chake cha sheria namba 16 ambacho waharamia wa uchumi watakaokamatwa nchini katika bahari ya hindi watafunguliwa mashitaka katika mahakama zake hapa hapa nchini na wala sio kama ilivyokuwa mwanzo kufunguliwa mashitaka katika mahakama za nchi nyingine mbalimbali barani Afrika kitendo kilichosababisha kuleta na kusababisha uharamia kushamiri sana katika bahari hiyo ambapo wahusika walitambulika kutoka katika nchi ya Somalia.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za wizara hiyo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh.Bernard Membe amesema, serikali inashughulikia swala hili na kwamba italikamilisha kwani hapo mwanzo waharamia waliokuwa wakikamatwa katika bahari hiyo walihukumiwa nje ya nchi husika kitendo ambacho kilisababisha uharamia kushamiri kwa nguvu katika bahari ya hindi.

No comments:

Post a Comment