Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Wednesday, June 9, 2010

Waandishi nawaomba msiandike habari za uzushi- Wassira



WAZIRI wa kilimo, chakula na ushirika, Stephen Wassira, amesema kuwa kuekelekea katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu, baadhi ya waandishi wa habari, wamekuwa na tabia ya kununuliwa na watu ambao utangaza nia ya kugombea, ambapo kwa makusudi kabisa uamua kuandika habari za uzushi na ambazo ni za kuleta machafuko ndani ya jamii.

Waziri Wassira aliyasema hayo mjini Bunda wakati akihutubia kwenye mkutano wa hadhara, ambapo alisema kuwa baadhi ya waandishi wa habari wanaharibu taaluma hiyo kwa kuandika maneno ya uchochezi ndani ya jamii.

Alisema kuwa tabia hiyo aiendani kabisa na maadili ya uandishi wa habari ambapo aliwaomba waandishi hao kuaachana na tabia hiyo bali wandike habari zilizo za kweli kwani taaluma ya habari ni kitu muhimu sana kwa maslahi ya taifa.

‘Kuna baadhi ya wandishi wa habari wanaikuka maadili ya kazi yao……mtu anaamua kutunga uongo kabisa…mtu ni mwandishi wa habari anaka Mugumu lakini analala Bunda, kazi yake kuandika chuki tupu, mpoaka najiuliza huyu naye analala huku analipiwa nani Mungu wangu, na hii kazi anayoandika ya chuki anataka apate faida gani kwa chuki hiyo, mambo ya ajabu wala hayatakiwi kuyarudia, maana mengine hayatakiwi kutoka kwenye kinywa cha mtu mwenye hekima…mtu mmoja ana majina mawili kesho anaandika hili leo hili’

Waziri Wassira ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Bunda, aliwataka watu wanaotangaza nia ya kugombea nafasi mbalimbali kuacha tabiya ya kutumia waandishi wa habari kuandika habariza uchochezi ambazo zinaweza kuleta athari kubwa katika jamiii, na badala yake watowe sera zuri na waje na hoja maalumu ya kumletea maendeleo mwananchi.

Alisema kuwa waandishi wa aina hiyo wanaharibu sifa nzuri ya wilaya ya Bunda, kwani kuandika uongo ni kutaka kuleta machafuko ndani ya jamii, ambapo kwa Bunda kitu hicho ni kigeni.

No comments:

Post a Comment