Habari mbalimbali toka pande za bongo bila kusahau matukio mbalimbali yanayorindima pande zote za dunia
Psquare Ft. J.Martins- E No Easy
Wednesday, June 9, 2010
Mawaziri wapya watangazwa Japan!
Waziri mkuu mpya wa Japan Naoto Kan ametangaza baraza lake lipya la mawaziri huku mwanasiasa mkuu wa mrengo wa kushoto Yoshiko Noda akishikilia wadhifa wa waziri wa fedha kama ilivyotarajiwa.
Viongozi wote hao wanaazimia kupunguza sehemu kubwa ya deni la taifa hilo. Wadhifa zingine zilipewa mawaziri waliokuwepo katika baraza la zamani. Bwana Kan alichukua wadhifa huo baada ya kujiuzulu kwa aliyekuwa waziri mkuu Yukio Hatoyama, kutokana na mzozo juu ya kambi ya kijeshi ya Marekani katika kisiwa cha Okinawa.
Umaarufu wa chama tawala cha Democratic ulididimia chini ya uongozi wa Hatoyama na wadadisi wanasema kuwa kuna matumaini kiongozi huyo mpya atasaidia kukikomboa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment