Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Saturday, June 12, 2010

Namba za ZNZ sasa Kimeo Bara!Wale wenzetu na sie tuliojinunulia magari yetu ya bei chee Zenji (Zanzibar)..na kutanua kiulaini mjini na namba za huko za 'ZNZ' zilizokuwa zikitumika kitambo kidogo kabla hatujajiandaa kubadilisha namba hizo kwa kulipia kodi,tunaelezwa na TRA kuwa hatima yetu imefikia kikomo.

Mamlaka hiyo ya mapato (TRA) inadai kuwa imebaini kuwa kwa kutumia namba hizo zilizokuwa zikitumika na ndugu zetu wa kisiwani kitambo kilichopita...kabla hawajaingia kwenye mfumo wa namba kama za kwetu bara...tunakuwa tunakwepa kodi...na kutokana na hilo imetoa mwezi mmoja kwa wale wote wanaotumia namba hizo kuzisajili mara moja kabla bakora hazijaanza kutembea mitaani hahaha.

Ofisa Uhusiano Mkuu wa TRA, MacDonald Mwakasendile, alisema jana kuwa hatua hiyo inatokana na kuwapo mitaani kwa vyombo hivyo; magari, pikipiki na vingine ambavyo vina namba za usajili za ZNZ huku wamiliki wakijua kuwa wanakwepa kodi kwa kuwa hakuna wanakolipia maana namba hizo hazitumiki hata Zanzibar.

“Hatutaki kusumbuana na watu, tumewapa muda, maana mwingine anaweza kulalamika hakuwa anajua japo sheria inamtaka kufanya hivyo, mwezi mmoja unatosha na hatua nyingine zitachukuliwa maana mtu unaponunua gari au pikipiki, unapaswa ibadilishwe mara moja namba za usajili,” alisema.

Kwa mujibu wa tangazo la TRA lililotolewa na Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, kupitia vyombo vya habari jana, wahusika wanapaswa kuwa wameandikisha kwa mujibu wa Sheria ya Usalama Barabarani kifungu namba 30 cha mwaka 1973.

No comments:

Post a Comment