Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Wednesday, June 2, 2010

Manji alipia wanachama 3,000 Mechi ya Brazili!!


Mfadhili mkuu wa Klabu ya Wanajangwani Yanga Yusuf Manji, ametoa zaidi ya Tsh. Milioni 90 kwa ajili ya kuwalipia Wanachama wa Klabu hiyo wanaozidi 3,000, kwa ajili ya kushuhudia mpambano kai ya Kikosi cha timu ya Taifa ya Brazili na Taifa Stars.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la kandanda nchini TFF Fredrick Mwakalebela amethibitisha kupokea kiasi hicho cha fedha kutoka kwa mdhamini huyo wa Yanga, alipokuwa akielezea masuala ya michezo nchini mbele ya Wanahabari.

Wakati huo huo Msemaji wa TFF Florian Kaijage amesema tiketi za kushuhudia mpambano huo zitaanza kutolewa kuanzia Alhamisi Mchana wiki hii na kwamba maombi ya jukwaa la VIP A tayari yamezidi idadi ya nafasi iliyopo na kuwataka wadau kujaribu VIP zilizosalia na majukwaa mengine

No comments:

Post a Comment