Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Thursday, June 3, 2010

Mtikila ashikwa pabaya!


MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala imekataa ombi la Mwenyekiti wa Chama cha Democratc Part (DP) Mchungaji Christopher Mtikila la kutaka kuanza kusikilizwa upya kwa kesi inayomkabili ya madai ya sh milioni 9.8.

Juni 14 Mtikila atatakiwa aieleze mahakama ni kwa nini asifungwe, kwa kawaida kifungo cha madai huwa hakizidi miezi sita.

Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Joyce Minde amefuta ombi la kuanza kusikilizwa kwa kesi hilo kwamaelezo kwamba liliwasilishwa nje ya muda.

Minde amemtaka Mtikila amlipe mlalamikaji gharama za usumbufu kwa kuwa mshitakiwa huyo amekuwa na tabia ya kutofika Mahakamani siku za kesi.

Kesi hiyo inawakabili washitakiwa wawili, Mtikila na Mariam Issa.

Mtikila na mwenzake wanadaiwa kukopa sh milioni 9.8 kwa mfanyabiashara Paskazia Matete kwa makubaliano kuwa wangemlipa na riba lakini hawakufanya hivyo.

No comments:

Post a Comment