Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Saturday, June 12, 2010

Wachungaji, Sheikh Nusura wapeane mangumi!!


SAKATA la kuzika mwili wa mtoto wa Mchungaji wa Kanisa la FPCT, Maria Yona (19) aliyefariki baada ya kuchinjwa kama kuku na mama yake mdogo limeingia katika sura mpya baada ya wachungaji pamoja na Sherkh mmoja kutunishiana misuli.

Hatua hiyo imekuja siku moja kufuatia wananchi kugoma kuzika mwili wa mtoto huyo hadi pale uchunguzi wa siku tano kufanyika.

Mabishano baina ya wachungaji wa kanisa hilo na sherkh mmoja aliyejulikana kwa jina la Mti Mkali kufika nyumbani kwa baba yake mzazi ili kufanya miujiza.

“Mchungaji pamoja na familia yake walikubali kundi hilo kuingia ndani ili kuona mwili wa marehemu lakini kundi la wachungaji wa kanisa la FPCT waligoma kabisa watu hao wasiingie ndani ya nyumba ya hiyo.”

Mwenyekiti wa kijiji hicho Bw.Aron Joseph alisema mara baada ya kundi hilo kutaka kuingia ndani ili kuuona mwili wa marehemu ndipo wachungaji waligoma na kuwaamuru kundi hilo kuondoka katika eneo hilo .

Kundi hilo pamoja na wananchi zaidi ya 3,000 waliokuwepo nyumbani hapo ili kushuhudia miujiza hiyo walipigwa na butwaa baada ya kuona kuwa watu hao wamezuiwa na wachungaji kufanya kazi yao .

Alisema kundi la Mti Mkali waliamua kuondoka katika eneo hilo na kuacha wananchi wakiwa katika makundi makundi kila moja likitafakari nini cha kufanya.

Bw.Joseph alisema hatua ya kutokuzika mwili wa mtoto huyo ambaye alikuwa mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Makhojoa, awali ulileta kasheshe wengi wa wananchi wakitaka usizikwe mpaka uchunguzi ufanyike.

Alisema ndipo wananchi walikusanyika katika makundi matatu kundi la vijana, kinamama na wazee kila moja likipewa majukumu ya kutafakari nini kifanyike.

Mara baada ya makundi hayo kukaa pamoja na kuleta mrejesho wa makubaliano ilionekana kila kundi lilitaka uchunguzi wa kina ufanyike kwani mazingira ya kifo cha mtoto huyo ni ya utata.

Hata hivyo ndipo ulizuka mjadala kijijini hapo ambapo wachungaji wa kanisa la FPCT, waislamu pamoja wa wazee waliingia katika maombi maalum ili kubaini chanzo cha kifo hicho.

Bw.Joseph alisema katika maombi hayo ndipo muumini wa kanisa la FPCT mwanamke mmoja alisema ameona maono kuwa Maria hajafa bali amefichwa sehemu na kwamba kilichopo ndani sio maiti bali ni gogo.

Alisema mwanamke huyo ambaye hata hivyo hakuweza kumtaja jina, juzi katika mkutano baina ya mkuu wa Wilaya ya Singida Bw.Pascal Mabiti na OCD Bw.Ngunguru, alisema kuwa katika maombi yake, maono yake yanaonesha kuwa hakuna mtu aliyekufa katika nyumba ya mchungaji Yona Mbighii.

Hapo ndipo wananchi walimtaka kutoa ushuhuda wake kwenye mkutano huo kwamba amwemwona wapi Maria, ndipo viongozi wa dini pamoja na wazee walikubaliana kuwa amweleze DC maono yake hayo kwa siri.

“Hapo ndipo huyu mama alimnong’oneza DC juu ya maono yake na ndipo mkuu wa Wilaya pamoja na OCD walisema kuwa suala hilo watalishughulikia kisheria lakini marehemu azikwe.”Alisisitiza Mwenyekiti huyo wa kijiji.

“Lakini jambo la kushangaza ni kwamba jana asubuhi mwanamke huyo alitoweka hapa kijijini na hajulikani alipo na juhudi za kumtafuta bado zinaendelea ili aweze pia kuweka bayana maono yake hayo mbele ya wananchi wa kijiji hiki.”Alisistiza.

Baada ya mabishano ya siku nzima ndipo iliamuliwa kwamba mwili huo uzikwe, jambo ambalo wananchi walipinga na kuamua kumziria mchungaji Mbighii na kanisa lake marehemu ili waamue wenyewe kamawatazika au la lakini wananchi hawapo tayari kushiriki mazishi hayo.

Alisema baadae wachungaji pamoja na baadhi ya ndugu wa marehemu, waliuzika mwili wa mwanafunzi huyo jana majira ya saa 4:00 asubuhi maziko ambayo yalihudhuriwa na watu takribani 30 tu.

Mwanafunzi huyo ambaye ni mtoto wa mchungaji wa Kanisa la FPCT lililopo katika kijiji cha Mipilo Tarafa ya IIongero, Halmashauri ya Wilaya ya Singida aliuawa kikatili juni saba mwaka huu na mama yake mdogo kwa kukatwa shingo kama kuku kutokana na imani za kishirikina

No comments:

Post a Comment