Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Wednesday, June 2, 2010

Bwana harusi mtarajiwa apewa kipigo cha uhakika!
Kijana mmoja aliyetajwa kwa jina moja la Shauri, ambaye ilielezwa kuwa hivi karibuni alipeleka barua ya posa maeneo ya Buguruni, alinusurika kuuwawa baada ya kumkwapua mtu simu maeneo ya Kariakoo, katika mitaa ya Aggrey na Max Mbwana na kisha kupewa kipigo cha 'mbwa mwizi.

Wakati akipata mkong'oto wa nguvu kutoka kwa raia wenye hasira, kijana mmoja alisikika akisema kuwa mwizi huyo anamfaham baada ya kuleta barua ya posa mitaa ya kwao Buguruni.

"Huyu jamaa namyaka kwa sana, hivi karibuni alileta barua ya posa pale kwa jirani yangu Buguruni, anatarajia kumuoa dada mmoja aitwaye Zainabu Abulrahman, loo..! kumbe ni kibaka?" alisikika kijana huyo akishangaa.

Kibaka huyo, ambaye ilikuja kuelezwa baadae kuwa ni mzoefu wa kukwapua na kupewa kipigo mitaa hiyo alisalimika japo aliondoka huku mwili ukiwa umelowa kwa damu…!!

No comments:

Post a Comment