Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Wednesday, June 2, 2010

Marmo aangukiwa na CCJ!


CHAMA Cha Jamii CCJ kimemshukia Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu(Sera,Uratibu na Bunge) Philip Marmo, kwa kutumia ofisi yake vibaya kwa kuingilia ofisi ya Msajili pamoja na Chama na kumuita ni sawa na mpiga debe vituo vya basi.

Kauli hiyo imetolewa leo na Naibu Katibu Mkuu Bara, Dickson Ng’hily katika makao makuu ya chama hicho Mwananyamala jijini Dar es Salaam,kufuatia taarifa zilizoripotiwa katika vyombo vya habari juu ya CCJ kutopatiwa usajili wa kudumu kwa kuchelewa kufanya hivyo.

Nghily alisema kwa kauli alizotoa Waziri Marmo ni za kichochezi kwa Watanzania wapendamaendeleo hasa katika dhama hizi za ukweli na uwazi.

“Kauli aliyoitoa kwa kiongozi kama yeye ni ya kipuuzi na isiyo na mantiki kwa watanzania, yeye hana mamlaka ya kumsemea msajili wa vyama, kufanya hivyo ni sawa na mpiga debe na mvurugaji wa ukweli” alisema Nghily.

Aliendelea kusema kuwa, kwa taarifa alizonukuliwa waziri huyo ikiwemo ya Tendwa anaonewa, alidai kuwa yeye ndiye anayemuonea Tendwa kwa kuingilia mamlaka yasiyo muhusu.

“Marmo ndiye anayemuonea Tendwa kwa kumuingilia ofisi yake, Ofisi ya Msajili hipo huru iweje Waziri kama yeye aingilie chombo hicho huru?” alihoji na kutolea mfano kuwa, Marmo anamfunika Tendwa pastiki alafu anamwambia apite katika moto pasipokujua madhara atakayoyapata; alimalizia.

No comments:

Post a Comment