Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Sunday, June 6, 2010

Sasa hivi ni Ubabe kwa kwenda mbele, Hatuonei mtu huruma-Tanesco!


Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), limesema kuanzia sasa litaanza kutumia ubabe kukata umeme katika taasisi mbalimbali za serikali zinazodaiwa na shirika hilo.

Taasisi pekee zitakazonusurika na hatua hiyo ni hospitali tu na kwamba lengo lao ni kukusanya deni la Sh300 bilioni kutoka kwa wateja wao.

Hivi karibuni Tanesco ilikaririwa ikisema inadai wateja wake wake jumla ya Sh300 bilioni zikiwa ni malimbikizo ya madeni ya ankara za kila mwezi.

Kwa mujibu wa Tanesco Sh58 bilioni kati ya hizo ni deni la taasisi mbalimbali za serikali na zilizobakia ni madeni ya watu binafsi.

Mkwara huo ulichimbwa jana na Ofisa Uhusiano wa Tanesco, Badra Masoud,ambapo aliweka wazi kuwa kuanzia sasa kutakuwa hakuna kujuana baina ya Tanesco na wadaiwa hao SUGU.

"Safari hii tutatumia nguvu kukata umeme kwa wadaiwa wote hata kama ni taasisi za serikali isipokuwa hospitali tu," alisema Badra.

"Kama ni hospitali inadaiwa tutakwenda kwa mara ya kwanza na kuueleza uongozi kwamba jamani mna deni la kiasi kadhaa, tulipeni.

Tutawapa muda kama ni wiki au mwezi lakini nao baada ya majadiliano hayo basi tutatumia nguvu kukata umeme ikiwa watashindwa kutekeleza ahadi," alisema Badra.

Badra alisema Tanesco imeandaa utaratibu mzuri wa kuepukana kujuana na kuwapo kwa rushwa baina ya wadaiwa na mafundi wa shirika hilo katika operesheni ya kukata umeme.

"Hakutakuwa na rushwa wala kujuana kwa sababu mafundi watakaopita Dar es Salaam kukata umeme watatoka mikoani na wale wa mikoani watatoka Dar es Salaam na mikoa mingine." alisema Badra.

"Kwa hiyo tutahakikisha kama taasisi au mtu akikatiwa umeme haurudi hadi atakapomaliza kulipa malimbikizo yake yote," alisisitiza Badra.

No comments:

Post a Comment