Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Saturday, June 12, 2010

Familia yaburuzana kwa sangoma!


Familia moja ya jijii imekumbwa na mgogoro mkubwa wa kutuhumiana hadi kufikishana kwa waganga wa kienyeji kupigiwa ramli baada ya mtoto wao kupotea katika mazingira ya kutatanisha.

Mtoto huyo, Deogratus Jumanne (6), mkazi wa Kiwalani, alipotea wiki mbili zilizopita baada ya kwenda kumsalimia bibi yake wa ukoo wa mbali, Binti Said, anayeishi Mbagala Kibonde Maji tangu Mei 20, mwaka huu, lakini ilipofika Mei 23, alitoweka nyumbani.

Wakati juhudi za kumtafuta mtoto huyo zikiendelea, familia hiyo iligawanyika makundi mawili ambapo mama mzazi wa mtoto, Nuru Seif, alikwenda kwa sangoma kushughulikia tatizo hilo lakini upande wa baba haukutaka kushiriki kwenda kwa sangoma.

Imedaiwa kuwa upande wa mama mtoto ulienda kwa waganga tofauti na kuambiwa kuwa mtoto huyo amechukuliwa na bibi yake mzaa baba anayejulikana kwa jina la Ester Nyagalu huku waganga wengine wakidai amechukuliwa na Binti Said wa Mbagala.

Kauli za waganga hao zilisababisha vurugu kubwa baada ya mama mzazi wa mtoto na ndugu zake, akiwamo kaka yake, Hashimu Seif, kumvamia bibi Nyagalu na kumtaka kuwapa mtoto ndani ya siku tatu.

Hata hivyo, siku tatu walizotoa ziliisha juzi huku bibi huyo akiwa kitandani akiumwa.

Kutokana na vurugu hizo, watoto wa bibi Nyagalu, ambao ni Job Nyagalu na Jumanne Loki, waliingilia kati kupinga kumhusisha mama yao mzazi na mambo ya kishirikina kuhusu upotevu wa mtoto wao huku wakidai kuwa aliyehusika ni bibi wa Mbagala, Binti Said.

Kwa mujibu wa baba mazazi wa mtoto huyo, Loki, alisema kwa mujibu wa maelezo ya binti Said alidai kuwa Mei 23, mwaka huu kulikuwa na sherehe jirani yake huko Mbagala ambapo ngoma za asili zilikuwa zikipigwa kuzunguka maeneo mbalimbali na inawezekana mtoto huyo alifuatana ngoma hizo na kushindwa kurudi kutokana na ugeni wa mazingira hayo.

Alisema kitendo cha mke wake kwenda kwa waganga kwa kushirikiana na ndugu zake huku wakimhusisha mama yake mzazi kilimkera sana ingawa awali aliamini kuwa huenda waganga wangebaini mtoto huyo alipo.

No comments:

Post a Comment