Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Wednesday, June 2, 2010

Serikali kununua Rada nyingine tena


Baada ya manunuzi ghali ya Rada ya ulinzi yaliyozua utata katika Serikali ya awamu iliyopita kutokana a mazingira yaliyozunguka mchakato wake, Serikali imetangaza tena kununua rada nyingine, safari hii ikihusishwa na suala la hali ya hewa.
Hayo yameelezwa na Waziri wa miundombine Dr. Shukuru Kawambwa katika ufunguzi wa mkutano wa Mafunzo ya Wataalamu wa hali ya Hewa wa baadhi ya nchi za SADCC yanayoendelea katika jiji la Dar es Salaam.

Waziri Kawambwa ameeleza kuwa Serikali ilitenga fedha katika bajeti mbalimbali na kufanikiwa kununua rada ya kwanza inayotumika hivi sasa, na kuongeza kuwa bado Serikali inatenga fedha katika bajeti zake ili kufanikisha azma hiyo ya kununua rada hiyo aliyoeleza itasaidia kuimarisha hali ya vipimo vyetu vinavyopima hali ya hewa.

Wataalamu hao wa mamlaka za hali ya hewa kutoka nchi za Anola, Msumbiji, Botswana, Zambia na wenyeji Tanzania, wamelenga kujadili matatizo mbalimbali ya hali ya hewa na anga kwa ujumla katika ukanda huu wan chi za SADCC.

No comments:

Post a Comment