Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Monday, June 14, 2010

Wafukua kaburi na kuiba viungo vya albino!


Watu wasiojulikana wamefukua kaburi alimozikwa mlemavu wa ngozi (albino) usiku wa manane wilayani Biharamulo na kuondoka na mkono na mguu wake huku masalia mengine yakiachwa ndani ya jeneza juu ya kaburi lake.

Habari kutoka eneo la tukio mkoani Kagera, zinaeleza kuwa tukio hilo lilitokea usiku wa kuamukia Juni 10, mwaka huu katika Kijiji cha Nyakashenye wilayani Biharamulo.


Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi mkoani Kagera,kaburi lililofukuliwa ni la Lightness Laurian (29) alifariki dunia Januari mwaka huu.

Alisema watu hao walifukua kaburi na kutoa jeneza lake kisha wakalifungua na kuchukua viungo walivyovihitaji na kuondoka navyo.

Jeshi la polisi mkoani humo linaendesha msako mkali kuwasaka watu waliohusika na hadi sasa hakuna mtu anayeshikiliwa kuhusika katika tukio hilo.

No comments:

Post a Comment