Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Tuesday, June 8, 2010

Mkutano wa ECOWAS kuhusu usalama na usuluhishi wa mgogoro wafanyika nchini Nigeria!Mkutano wa 27 wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi ECOWAS kuhusu usalama na usuluhishi wa mgogoro unaendelea huko Abuja, Nigeria.

Kwenye mkutano huo wa siku 2 mwenyekiti wa kamati ya ECOWAS Bw. James Victor Gbeho amesema, eneo la Afrika magharibi liko kwenye kipindi muhimu cha mabadiliko ya mamlaka, ambapo hali ya usalama wa eneo hilo inakabiliwa na changamoto nyingi, kwa hiyo mkutano huo utazihimiza Niger, Guinea, Guinea Bissau na Togo zitulize migogoro yao, na kuihimiza Cote d'Ivoire ifanye uchaguzi mkuu, ambao umeahirishwa mara nyingi.

Kwenye mkutano huo mjumbe maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kwenye eneo la Afria magharibi Bw. Said Djinnit amesema, Umoja wa Mataifa utaimarisha ushirikiano kati yake na ECOWAS, na kuhimiza amani ya kudumu na maendeleo katika eneo la Afrika

No comments:

Post a Comment