Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Wednesday, June 2, 2010

Watoa misaada ya kibinadamu wawekwa jela na utawala wa Israeli



Utawala wa Kizayuni wa Israel umewahamishia gerezani watu wasiopungua 610 waliokuwa kwenye meli zilizokuwa zikipeleka misaada ya kibinadamu katika eneo la Ukanda wa Gaza. Taarifa zinasema kuwa, wafikishaji misaada na watetezi wa haki za binadamu hao wamepelekwa kwenye gereza la Biirul Sab'aa lililoko kusini mwa Palestina inayokaliwa kwa mabavu.

Kabla ya hapo viongozi wa utawala wa Israel walitangaza kuwa, ni watu 480 tu wa kutoa misaada ya kibinadamu ndio waliopelekwa kwenye gereza hilo kwa ajili ya kusailiwa na waliosalia hawajulikani walipo. Utawala huo ghasibu umetangaza kuwa watu wengine 45 wengi wao wakiwa ni raia wa Uturuki wamepelekwa hospitalini baada ya kupata majeraha yaliyosababishwa na shambulio lililofanywa na makomandoo wa Kizayuni dhidi ya meli ya misaada, na kusababisha watu 20 kupoteza maisha yao.


Wakati huohuo, nchi mbalimbali duniani zimetoa radiamali zao kuhusiana na shambulio liliofanywa na Wazayuni dhidi ya meli za misaada ya kibinadamu. Kristen Halvorsen Waziri wa Elimu ambaye ni kiongozi wa mrengo wa kushoto wa chama cha Kisoshalisti nchini Norway ameitaka jamii ya kimataifa kuuwekea vikwazo vya biashara ya silaha utawala huo ghasibu.

No comments:

Post a Comment