Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Saturday, June 5, 2010

UFARANSA YATOA BILIONI 52.5 KUBORESHA SEKTA YA MAJI NCHINI


Serikali ya nchini Ufaransa kupitia mtekelezaji wake katika sekta ya maji yaani shirika la maendeleo la kifaransa (AFD) wamesaini mkataba wa kutoa mkopo wa Euro milioni 30 ambapo ni sawa na fedha za Kitanzani shilingi bilioni 52.5 kwa serikali ya Tanzania katika kusaidia sekta ya maendeleo ya maji (WSDP) kutoa maji safi kwa watanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kusaini mkataba huo balozi wa Ufaransa nchini Bw. Jacques de LABRIOLLE amesema (AFD) limefadhili miradi miwili ya maji katika miji ya Utete na Mpwapwa inayohusika na uzalishaji wa maji,usafirishaji na ugawaji wa maji ambapo miradi hiyo inategemewa kumalizika mwezi huu wa Juni pamoja na mingineyo iliyoko miji ya Bukoba na Musoma inayotarajiwa kuanza mwanzoni mwa mwaka ujao.

Aidha Bw. Jacques amesema mkopo huu ni maalum kwa kuwa masharti yake ni nafuu wenye riba ya asilimia 1 ambao una marejesho ya miaka 25 amapo pia amesema mkopo huu sio kwa ajili ya miradi maalumu bali ni mchango kwenye mfuko wa maji unaofadhiliwa na nchi wahisani na kwamba Tannzania inafungua ukurasa mpya wa misaada ya Ufaransa kwa kuongeza kiwango mara 5 zaidi ikiwa mkopo huu utatumika kikamilifu.

Akishukuru msaada huo katibu mkuu wa Wizara ya fedha na uchumi nchini Tananzania Bw.Ramadhan Khijjah amesema mfuko huu wa (WSDP) unasaidiwa na nchi nyingi ikiwemo benki ya dunia,Ujerumani,Jicca ili kuweza kusaidia upatikanaji wa maji katika miji 19.

No comments:

Post a Comment