Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Thursday, June 3, 2010

Waasi 16 wa LRA wauawa


Jeshi la Uganda limesema ,limewaua waasi 16 wa kundi la Lord´s Resistance Army LRA, katika mapambano yaliyotokea Jamuhuri ya Afrika ya Kati.

Msemaji wa jeshi la Uganda, Luteni Kanali Felix Kulayigye amenukuliwa na Shirika la Habari la Ujerumani DPA, akisema kuwa wapiganaji hao wa LRA waliuawa wiki iliyopita.
Amesema kuwa jeshi la Uganda linaendelea kuwasaka wapiganaji hao wa LRA ambao wamekimbilia katika misitu ya Jamuhuri ya Afrika ya Kati.

Serikali za Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Afrika ya Kati pamoja na Uganda zilitilia saini makubaliano ya kuwasaka waasi hao wa LRA.

No comments:

Post a Comment