Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Sunday, June 13, 2010

Barabara zetu zimezidi uchakavu, walalama wanaTabata!!


Wakazi wa Tabata wameilalamikia Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kufumbia macho suala la barabara chakavu zilizopo katika mitaa ya maeneo yao, kama ilivyo kwa barabara ndogo ya Savannah Relini yenye madimbwi makubwa ya maji, yanayoifanya isipitike.

Akielezea hali ya Barabara hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Mazingira wa Kimanga Darajani Florence Mashaka, amesema madimbwi ya maji katika barabara hiyo ya Savannah Relini yamekuwa hapo kwa miaka 2 sasa, na pindi mvua zinaponyesha hali huwa mbaya sana.

Amesema Barabara hiyo husaidia kupitisha magari ya Vingunguti, Segerea, Ubungo, Kinyelezi na Buguruni nyakati za asubuhi na jioni, katika kipindi ambacho Barabara kuu ya Mandela inapokuwa imefurika magari.

Nao wajumbe wengine wa Kamti ya Mazingira sambamba na mkazi mmoja wa eneo hilo Paul Balua, wameitaka Manispaa kujitokeza mara moja kuokoa barabara hiyo, ili kuwezesha shughuli za watu kufanyika.

No comments:

Post a Comment