Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Monday, June 7, 2010

TV kutoonyesha live mechi ya Brazili na Stars!!


Shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF, limebainisha kutokuwepo ruksa kwa televisheni za ndani kuonyesha live mpambano wa kirafiki baina ya Taifa Stars na Brazili, kutokana na umiliki wa haki hiyo kuwa ni wa nchi ya Brazil pekee kupitia televisheni yake ya Global TV.

Akielezea sakata hilo leo kwa Wanahabari hapa jijini Dar es Salaam, Katibu mkuu wa TFF Fredrick Mwakalebela amesema Tanzania haina haki miliki ya kuonyesha mechi hiyo kupitia televisheni zake na kwamba kuna kikwazo cha kisheria kinachoiruhusu Brazili tu kuirusha mechi hiyo.

Amesema uamuzi huo wa Brazili umetoa fursa kwa televisheni kurekodi mchezo huo kisha kuonyesha baadaye kama marudio, lakini si kuonyesha moja kwa moja (live coverage).

Wakati huo huo tiketi za kushuhudia mpambano huo zimeelezwa kupatikana katika vituo vya Mlimani City, viwanja vya Biafra, Mnazi mmoja pamoja na ndani ya uwanja wa Uhuru tu.

No comments:

Post a Comment