Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Thursday, June 3, 2010

Mzingiro wa Gaza uondolewe, Asema Raisi wa Iran!


Rais Mahmoud Ahmadinejad amesema kuna ulazima wa jamii ya kimataifa kuchukua hatua za kuondoa mzingiro dhidi ya Gaza. Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa mwito huo katika mazungumzo kwa njia ya simu aliyofanya na Ismail Haniya, Waziri Mkuu wa serikali halali ya Palestina.

Katika mazungumzo hayo, mbali ya kulaani shambulio la utawala wa kizayuni dhidi ya msafara wa meli zilizobeba misaada ya kibinaadamu, Rais Ahmadinejad amesema jamii ya kimataifa inapaswa kuanzisha harakati maalumu na kuongeza maradufu juhudi zake za kuondoa mzingiro uliowekwa dhidi ya Gaza.

Aidha ametangaza kwa mara nyingine tena mshikamano wa taifa la Iran na wananchi wa Palestina na kubainisha kuwa Iran inawaunga mkono kikamilifu wananchi wa Palestina na wale wanaowaunga mkono wananchi hao. Wakati huo huo shehena ya kwanza ya misaada ya kibinaadamu iliyotolewa na wananchi wa Iran itasafirishwa hivi karibuni kwa ajili wananchi wa Palestina wa eneo la Ukanda wa Gaza.

No comments:

Post a Comment