Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Sunday, June 13, 2010

Watani wa Jadi kufinyana Agosti 14!



Agosti 14 ndani ya jiji la Lukuvu, ni siku ya ile mechi maalum ya kuwania ngao ya hisani kwa Watani wa jadi Simba na Yanga.

Naye Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Florian Kaijage alisema kwamba timu hizo zitakutana baada ya Watoto wa Msimbazi 'Simba' kunyakua Ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu uliopita huku mahasibu wao wa jadi Yanga walimaliza wakiwa washindi wa pili wa ligi hiyo.

Alisema mbali na mechi hiyo, pia kutakuwa na mechi za kuwania ngao ya hisani katika mikoa yote nchini ambapo bingwa wa kila mkoa atacheza dhidi ya mshindi wa pili.

Kwani mwaka jana TFF iliwateua Mtibwa Sugar kutoka Morogoro kucheza dhidi ya mabingwa wa bara wa wakati huo, Yanga, baada ya Simba waliokamata nafasi ya pili huku Yanga kutoafiki kuvaana kwa madai kwamba hawakupewa taarifa mapema.

Mtibwa waliwachapa watoto wa jangwani 'Yanga' na kutwaa ngao hiyo ambayo huwaniwa wiki moja kabla ya kuanza kwa msimu wa ligi.

Na Agosti 21 mwaka huu ni kipindi cha kuanza kwa ile Ligi Kuu ya Tanzania Bara na itakuwa ni kipindi cha usajili wa wachezaji wapya

No comments:

Post a Comment