Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Saturday, June 12, 2010

Waganga wa jadi wampigia magoti Pinda!


Chama cha Waganga wa Dawa Asilia Tanzania, kimempigia magoti bosi wa mawaziri , Mizengo P, kuwaonea huruma na kuwapa kibali ili waendelee kutoa huduma kwa wateja wao kama ilivyokuwa siku za nyuma.

Hayo yaliwekwa wazi na chairman wa waganga hao, Simba Simba,ambapo alisema hatua ya serikali kuwasimamisha kwa muda usiojulikana, imewaathiri zaidi kwa vile ndiyo sehemu yao ya kupata fedha za kuendesha maisha.

Kwa mujibu wa Simba,wananchi wengi wamekuwa wakipata taabu kupata huduma hiyo, hali ambayo imepelekea kuwepo kwa waganga wanaotoa huduma hiyo kwa siri katika maeneo mbalimbali.

Alisema, kuwepo na misingi au chombo cha kuwaunganisha waganga wote nchini kutasaidia kuwasiliana katika kufanya kazi zao na kuwabaini waganga wanaojihusisha na vitendo vya kuwaua watu wenye uelemavu wa ngozi (albino).

Alisema chama hicho kimeweka taratibu ambazo zitawapa miongozo ya kazi waganga wote watakaojiunga kwenye chama chao ili watambuliwe kuanzia ngazi ya kata, mtaa, kijiji, wilaya mpaka taifa.

No comments:

Post a Comment