Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Wednesday, June 9, 2010

Vibaka wafanya sherehe kwenye gemu la Brazil na Stars!Watu kutoka mataifa mbalimbali wakiwemo mapaparazi wa kigeni walioambatana na wazee wa samba 'timu ya Brazil', hakika hawatakosa cha kuhadithia wataporudi makwao...baada ya kujikuta wakiingia mitegoni mwa vibaka wa kibongo na kupoteza vitu vyao kadhaa zikiwemo pochi zao zilizokuwa na mikwanja ya kujikimu wakati wakiwa katika kazi yao nje ya Uwanja wa Taifa.

Sinema hiyo ambayo kwasisi watoto wa uswazi mara nyingi tumekuwa tukiistukia na kujiweka sawa,ilitokea muda mfupi kabla ya kuanza kwa mechi hiyo, wakati waandishi hao wakipiga picha nje ya uwanja, wakati huo watu wakiwa katika harakati za kuingia uwanjani kuzishuhudia Taifa Stars na Brazil.

Walichofanya vibaka hao ni kuwahadaa waandishi hao kwa kuwatisha kuwa kwanini wanapiga picha katika eneo hilo, wakati wakijaribu kujieleza, kibaka mmoja aliyekuwa nyuma ya mwandishi mmojawapo, akachomoa pochi na kukimbia.

Licha ya kuwapo askari eneo la nje ya uwanja, vibaka hao walitumia mbinu kali na kufanikiwa kutokomea, licha ya juhudi kubwa za askari polisi.


Tukio jingine ambalo nalo litabaki kama kumbukumbu isiyopendeza, ni kugoma kwa ‘CD’ ya wimbo wa taifa kwa kuimbwa nusu yake, tofauti na ule wa Brazil ambao uliimbwa hadi mwisho.

Hii imedhihirisha jinsi Tanzania ilivyo nyuma, kwani licha ya kuwapo kwa njia nyingi za kiteknolojia, lakini wimbo ya taifa hadi leo bado unahifadhiwa kwenye mfumo wa CD.

Baada ya CD hiyo kugoma, maelfu ya mashabiki waliokuwa uwanjani walishindwa kuvumilia kuonyesha hasira zao wazi, wakaamua kuzomea. Yote haya yanapaswa kuwa funzo kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na serikali kwa ujumla.

Kwa kuwa mechi ya Brazil ni ya kihistoria kwa Tanzania, hata maandalizi yake yalipaswa kuwa ya kiwango cha juu, tofauti na ilivyokuwa.

No comments:

Post a Comment