Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Sunday, June 6, 2010

Uchaguzi mkuu ujao ni Batili, Anena Mtikila!!



Wakati wakati wakiwa na shauku kutambua nini kitakuwa hatamu ya maamuzi ya Mahakama ya Rufaa kuhusu kesi ya mgombea binafsi, Mwenyekiti wa Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila a.k.a Msema Hovyo amedai kuwa uchaguzi mwaka huu bila mgombea binafsi utakuwa ni haramu na batili.

Mtikila pia amesema maofisa wa serikali na taasisi za serikali wanaohusika na kuzuia mgombea binafsi, kama Mwanasheria Mkuu na Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi wanapaswa kukamatwa na kushtakiwa kwa kosa la jinai la kuvunja katiba na matuizi mabaya ya madaraka kwa kuwa watakuwa wamekiuka amri halali ya mahakama ambayo ni sheria.

Akizungumza kwa jazba hapo jana, alisema kama Uchaguzi Mkuu ujao utafanyika bila kuhusisha mgombea binafsi hautakuwa uchaguzi halali na hata viongozi watakaopatikana watakuwa wameingia madarakani kwa njia ya mapinduzi ya serikali halali, hivyo watakuwa sawa na wahaini au maharamia, hivyo wanapaswa kukataliwa.

"Kinachofanyika sasa ni maandalizi ya uchaguzi batili, yaani si uchaguzi kabisa, ni sawa na watu kusaini mkataba wa kufanya uhalifu, mkataba ule unakuwa si halali tangu mwanzo na hakuna mahakama yoyote itakaoutambua na hiki ndicho serikali inachofanya kuwaingiza wananchi katika zoezi batili na haramu," alisema.

"Tunategemea kuwa uamuzi wa Mahakama ya Rufaa utachelewa kwa kuwa suala wanaloliamua ni suala nyeti linalogusa maslahi ya watu wengi, si Tanzania tu bali Afrika na duniani kwa ujumla, lakini tumegundua kuwa tamko la Mahakama ya Rufaa la Aprili 8, 2010 kuhalalisha maamuzi ya Mahakama Kuu juu ya mgombea binafsi lina nguvu kama sheria yoyote itungwayo na bunge," alisema.

Mchungaji Mtikila aliwataka maofisa wa serikali na mawaziri kama Bw. Philip Marmo, Bw. Bernard Membe, Bw. Rajabu Kiravu, Mwanashria Mkuu na wengine ambao wamekuwa wakitoa kauli za kuwachanganya wananchi kuwa uchaguzi mkuu hauwezi kuhusisha wagombea binafsi, kuacha mara moja kwani wanachokifanya ni ukiukaji wa maamuzi ya mahakama, jambo ambalo ni kosa kisheria.

No comments:

Post a Comment