Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Monday, May 31, 2010

AY kupiga Collabo na Sean Kingstone!!Habari zilizopo ni kuwa yule mwakilishi wa muziki wa Bongo Flava nje ya nchi Ambwene Yessayah anatarajia kuangusha mzigo na msanii Mkali toka Jamaica ambaye siku za karibuni alidondoka kufanya show ya nguvu nchini, si mwingine ni Sean KingStone.

Sean Kingstone mwenyewe akihojiwa na Radio mmoja nchini hivi karibuni alipoulizwa ni mwanamuziki gani ambaye anamtambua hapa bongo na angependa siku moja afanye nae kazi, jamaa bila kusita alisema AY.

“Nilipokutana na jamaa kweli alisema anavutiwa na kazi zangu, akaniomba tukapige colabo, ni mtu ambaye hana mapozi na ilikuwa nipige naye ngoma moja hapa Bongo lakini bahati mbaya Producer wangu, Hermy Bakawa amesafiri. Kwa kifupi amenipa moyo sana, nikienda huko natarajia kufanya maajabu,” alisema A.Y

No comments:

Post a Comment