Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Sunday, April 11, 2010

Abiria akosa nauli, amwomba dereva wa teksi “kumla uroda” mkeweREVA wa teksi wa Bolton, Uingereza, aliambiwa na abiria wake kutoka Poland kwenda “kulala” na mkewe ili kufidia nauli ya Paundi 10.50 ambazo alikuwa anadaiwa, lakini alipokataa ombi hilo, abiria huyo alimfukuza akiwa na panga akitaka kumdhuru.

Dereva huyo mwenye umri wa miaka 38 aliachwa akiwa amepagawa kwa woga wakati abiria wake huyo alipomwamuru kufanya hivyo.
“Nauli ilikuwa ni Paundi 10.50,” alisema dereva huyo ambaye hakutaka kutaja jina lake na kuongeza, kuwa “jamaa badala ya kulipa aliniambia niingie ndani nyumbani kwake kwenda kulala na mkewe.”

“Katika miaka kumi ya kazi ya udereva, hii ni mara ya kwanza abiria kunipa mkewe nifanye naye mapenzi badala ya kunilipa nauli,” alisema dereva huyo ambaye alikuwa amewachukua abiria wake hao nje ya baa moja huko Bolton, Ijumaa.

Dereva huyo ambaye alishituka kuambiwa hivyo na kisha kupiga king’ora na simu ya kuwaita madereva wengine, alibaini kwamba mwanamume huyo ambaye aliamini ni mtu wa Poland, alikuwa amekimbilia ndani ya nyumba yake na kurejea akiwa na panga lenye urefu wa sentimita 45.

“Aliniijia moja kwa moja na panga lake, ikabidi nichomoke mbio haraka,” alisema dereva huyo aliyekimbia na kumwacha mshambuliaji wake huyo ambapo alipiga simu polisi ambao walifika na kumtia mbaroni mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 37.

No comments:

Post a Comment