Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Thursday, April 22, 2010

AUNT EZEKIEL AKUTWA UKANDA WA MAKAHABAMsanii mwenye nyota ya kung’ara katika tasnia ya muvi Bongo, Aunt Ezekiel Gryson ‘Gwantwa’ amenaswa na kamera ya paparazi wetu akiwa katika ukanda hatari kwa upatikanaji wa machangudoa, jijini Dar, Amani limekusanya albamu nzima.

Tukio hilo lilijiri ‘naiti’ ya Jumamosi pembezoni mwa baa maarufu ya Meridian iliyoko Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Aunt alitia timu eneo hilo majira ya saa saba usiku akiwa ndani ya kivazi cha Casino ambacho ni kipensi cha rangi ya bluu na singlendi ya rangi ya chungwa yenye maandishi mbele yakisomeka Trandy.

Baadhi ya wateja walioonekana kukolea kileo walianza kumjadili staa huyo wa filamu kutokana na mavazi yake hayo na maeneo aliyopo ambayo makahaba hupiga kambi kuwinda wateja wao.

Walisema vyema kama baada ya kufika eneo hilo na kampani yake wangetulia mahali kimya mpaka muda wa kutoka kuliko kutangatanga.


“La, si Aunt huyu? Mavazi gani sasa! Wenzake huvaa Casino kama Las Vegas, yeye anakuja nayo huku K’ndoni (Kinondoni) haoni kama anajijumuisha na ‘madadapoa’ wa barabara hii? Afadhali wangekaa mahali kimya mapaka wakati wa kutoka,” alisikika akihoji chapombe’ mmoja aliyekuwa miongoni mwa watu waliokuwa wakimpiga chabo msanii huyo.

Mbali na Aunt, wenzake waliotimiza idadi ya watatu waliandamana naye na kulifanya eneo lote la baa hiyo kuwa na macho juu juu kwani walionekana kutoka kwenye kilevi kabla ya kupiga hema eneo hilo.

Ndipo paparazzi wetu mahiri aliposeti mtambo wake wa kamera yenye kuvuta picha kwa mbali na kuanza kuwafotoa ambapo walitawanyika huku na kule huku wakimkemea ‘fotografa’ huyo kwamba aache mara moja kitendo cha kuchukua picha zao kwa kuwa walivaa ‘kihasarahasara’.

Licha ya mafanikio ya kumpiga picha, Aunt aliweza kukimbia kila kona ya eneo hilo lengo likiwa kukwepa ‘lenzi’ ya kamera huku akiwa ameng’ang’ania kipochi kidogo kwa kukibana kwenye kwapa na simu aliyokuwa ameishika mkono wa kushoto.

Ilifika mahali Aunt aliamua ‘kama mmbwai mmbwai’ pale alipoamua kusimama na kumwambia paparazi, ananukuliwa: “Haya piga tani yako, we si unataka picha yangu nikiwa hivi, piga sasa!”

Usemi huo ambao huenda yeye alitegemea ungesitisha zoezi hilo ulimpa nguvu mpya, ari mpya na kasi mpya mpiga picha wetu kwa kumlenga kisawa sawa kitendo kilichomfanya Aunt ajue kuwa, kumbe mshikakamera huyo alikuwa pale kikazi zaidi.


Wakati tafrani hilo likiendelea, wenzake walishasevu ishu hiyo kwa kwenda kuingia ndani ya gari na kumwacha ‘stering’ wao, Aunt akipambana na ‘adui’.

Mpaka mwisho wa mkanda, Aunt alikuwa amechoka kwa zoezi la kukimbiakimbia na sasa akabaki akitweta kama mwanariadha wa Ethiopia aliyeshiriki mbio za Marathon kwa mara ya kwanza.

Utafiti wa gazeti hili umegundua kuwa, asilimia sabini na tano ya machangu katika jiji la Dar wanapatikana wilaya ya Kinondoni hasa maeneo ya Makaburini, ukanda wa Mango Garden, MK na baa ya Meridian kuelekea Komakoma.

Sehemu nyingine ni Bamaga-Mwenge, barabara yote ya Shekilango, nje ya Club ya Sun Cirro, Magomeni ya Kwamacheni na kwenye Club maarufu wilayani humo ndiyo maana Aunt kuonekana kuzagaa eneo lile na mavazi yale kuliibua maswali kibao.

chanzo globalpublishers

12 comments:

 1. dada jirekebishe we ni mzuri sana ukiwa bize msanii bila uchi uchi unapendeza zaidi,iga mfano wa nacy sumari

  ReplyDelete
 2. ipo siku yako utaokoka utavaa kwa heshima tunakuombea roho mtakatifu akutembeeleee pokea heshima kama mkristu usiishi kama kahaba,kwa nini umechagua maisha ya hivyo,kua msanii maarufu lazima ukae uchi?unata niinii?

  ReplyDelete
 3. wewe kaa uchi tani yako maisha ni yako usimuishie mtu fanya kitu moyo wako unacho penda

  ReplyDelete
 4. mastaaaa wa filamu wa kibongo wengi inavosemekan huo ndiomtindo wao

  ReplyDelete
 5. jamani we mdada rizika na kipato chako cha sanaa!!hivi kweli wewe ni gold diger?unajidhalilisha na unadhalilisha wasanii kwa ujumla!!haaa!!hebu badilika plz.

  ReplyDelete
 6. Duuuuuuuuuu! Kama wasanii wenyewe ndo hawa, filamu zao kwishnee!

  ReplyDelete
 7. kwa kweli dada yangu you have to change unawafundisha nn wadogo zako pls badilika ww ni kioo cha jamii

  ReplyDelete
 8. kama unaona ni vizuri kuvaa hivyo its ok its your life

  ReplyDelete
 9. My spouse and I stumbled over here different web address and thought
  I should check things out. I like what I see so now
  i'm following you. Look forward to going over your web page yet again.

  Here is my web page - books of ra

  ReplyDelete
 10. Right here is the perfect webpage for anybody who wishes to find out about this topic.
  You know so much its almost hard to argue with you (not that I actually will need to…HaHa).
  You definitely put a fresh spin on a topic which has been discussed for years.
  Great stuff, just great!

  Also visit my homepage - novoline app

  ReplyDelete
 11. Appreciate the recommendation. Let me try it out.


  Look into my webpage book of raw spielen

  ReplyDelete
 12. WOW just what I was looking for. Came here by searching for sizzling hot download

  Review my website; book of ra app samsung ()

  ReplyDelete