Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Thursday, April 29, 2010

Aomba Kupelekwa Rumande kwa kukosa elfu kumi ya faini!


Mkazi wa Magomeni jijini Dar es salaam, Juma Said, 35, ameieleza Mahakama ya Mwanzo ya Kariakoo kuwa ni heri aende jela kutumika kifungo cha miezi sita alichohukumiwa kutokana na kukosa Sh10,000 za kulipia faini.

Said alieleza hayo ijumaa wakati Hakimu Mwajuma Diwani kumuhukumu kifungo cha miezi sita jela au kulipa faini ya Sh 10,000 baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa na kete moja ya bangi.

Hakimu Diwani alitoa hukumu hiyo ya kifungo baada ya mtuhumiwa huyo, aliyekuwa amefikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza, kukiri kosa lake.

Wakati hukumu hiyo ikitolewa mara baada ya mshtakiwa huyo kukubali shitaka, Hakimu Diwani alisema kuwa Said hakutaka kuisumbua mahakama hivyo aliamuru alipe faini ya Sh 10,000 au kifungo cha miezi sita jela.

Hakimu huyo alimuuliza mshtakiwa huyo kama anacho kiasi hicho cha fedha alichotakiwa kulipa faini.

"Mama mimi sina hela hiyo ya kulipa ni bora niende gerazani," alisema Said ambaye sasa ataigharimu serikali angalau Sh270,000 za chakula kwa siku 180 atakazokuwa jela iwapo atagharimiwa Sh1,500 kwa mlo mmoja kwa siku.
Jibu hilo lilimfanya hakimu huyo aamuru akatumikie adhabu hiyo ya kifungo cha miezi sita jela.

Said alidaiwa mahakamani hapo kuwa Aprili 21, mwaka huu katika eneo la Upanga wilayani Ilala alikamatwa na ofisa wa polisi wa kituo cha Salender Bridge, Koplo Eustace akiwa na kete moja ya bangi wakati akijua kuwa hilo ni kosa la jinai.

No comments:

Post a Comment