Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Friday, April 16, 2010

Waajiri Sasa Lazima Kuajiri Walemavu!


Bunge limepitisha Muswada wa Sheria ya Watu wenye Ulemavu ambao pamoja na mambo mengine, unawataka waajiri wenye wafanyakazi 20 au zaidi, kuhakikisha asilimia tatu ya wafanyakazi hao wanakuwa ni watu wenye ulemavu.

Sheria hiyo pia inawataka waajiri wenye watumishi 50 pia kuajiri idadi hiyo ya watu wenye ulemavu; lakini wawe na sifa zinazostahili.

Kwenye sheria hiyo imefafanuliwa kuwa wale ambao wameajiri watu 20 wanatakiwa watoe taarifa mara moja kwa mwaka wakati walioajiri zaidi ya 50 iwe mara mbili, kwa Kamishna wa Ustawi wa Jamii.

Katika sheria hiyo, pia inawashawishi waajiri kutowaachisha kazi waajiriwa wenye ulemavu wakati wa kupunguza wafanyakazi na pia kuweka mazingira mazuri ya kuwezesha walemavu kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.

Naibu Waziri Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Aisha Kigoda, aliliambia Bunge jana kuwa Muswada huo unazitaka taasisi zinazotoa huduma za jamii kuhakikisha huduma inayotolewa inawafikia kirahisi watu wenye ulemavu.

Naibu Waziri aliongeza kuwa sheria inaeleza wazi kuwa litakuwa ni kosa kwa yeyote kumzuia mtu mwenye ulemavu kuingia katika jengo lolote la umma.

No comments:

Post a Comment