Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Monday, April 5, 2010

katibu mwenezi tawi la CCM urusi asimamishwa uongozi


Ndugu Salim Mfungahema
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Yah: KUSIMAMISHWA UONGOZI KWA KATIBU MWENEZI SERA NA ITIKADI: TAWI LA CCM MOSCOW-URUSI

Kamati siasa ya Tawi la CCM-Moscow kama kamati ya Maadili ya Tawi, imefanya mkutano wake wa dharura tarehe 1 April 2010 chini ya Mwenyekiti wa CCM Tawi , Mhe, Dr. Alfred Kamuzora Mjini Moscow-Urusi. Wajumbe 9 kati ya 12, walihudhuria mkutano huo, Sawa na 75%, na kuruhusu Mkutano kuendelea na agenda .

Katika mkutano huo, Kamati ya Siasa ya tawi imejadili kwa kirefu Mwenendo wa katibu mwenezi sera na itikadi wa tawi Ndg. Salim Mfungahema. Kamati ya Siasa ya Tawi ilipokea na kujadili taarifa za tuhuma zilizomkabili Ndg. Mfungahema akiwa kama kiongozi mwandamizi wa tawi kama ifuatavyo:

Kusambaza waraka wa uchochezi kwa wanachama kinyume cha Katiba ya Chama Cha Mapindizi na kuleta mgawanyiko ndani ya Tawi, pasipo kuwasilisha Waraka huo katika vikao husika vya Tawi ili Kujadiliwa kwa mujibu wa katiba ya Chama Cha Mapinduzi ibara ya 14(4), (5).
Kuwa na dharau, kutokuwa na Heshima na uadilifu kwa viongozi wenzake wa Tawi, kuwakashifu viongozi wenzake kwa hiyo kuvunja katiba ya CCM ibara ya 14 (7),.
Kueneza sera za Uongo, na Kubuni Mambo yasio ya kweli na kushindwa kutoa vilelezo yakinifu kutokana na mambo anayozungumza/kuyasikia. Kamati Imegundua ni Mwongo na mchonganishi na mwenye nia kuvuruga Ustaarabu wa Wanachama kwa Viongozi wao.
Kueneza taarifa za Uchochezi na chuki kwa wanachama na Viongozi wa Tawi.
Kuidanganya Kamati ya Siasa na Halmashauri kuu kwa hiyo kuvunja katiba ya CCM ibara ya 14 (4), Kujichukulia Madaraka binafsi bila Kufuata Katiba na Ushirika, kubadili tafsiri za Maamuzi pasipo viongozi wengine kufahamu.
Kwa kufanya hivyo na mambo mengine, Kamati ya siasa imeridhia kuwa Bwana Mfungahema amekiuka miiko ya uongozi kama ilivyoainishwa kwenye Katiba ya CCM, ibara ya 18 (1) (2) na ahadi za mwanachama ibara 8. Pia katika Mwongozo wa Tawi la CCM Moscow Vipengere vifuatavyo:,Masharti ya mjumbe wa kamati ya siasa ibara ya 1:1.5(a). Utendaji: ibara ya 8:1(d) na (e) na ibara ya 8:2 na 8:3 ya Mwongozo wa Tawi 2008.

Kwa hiyo basi, Pamoja na kushauriwa katika vikao mbali mbali vya Chama ngazi ya Tawi kwa kuzingatia miiko ya uongozi bila kubadilika, na kwa mujibu wa Katiba ya Chama Cha Mapinduzi ibara ya 39(9) kikao cha kamati ya Siasa kama kamati ya Maadili ya Tawi kimeona kuwa Bwana Mfungahema ameshindwa kutimiza matarajio ya wanachama zaidi ya kuzalisha migogoro ndani ya Tawi. Kwa kuzingatia hilo, Kamati ya Maadili katika kikao chake kilichokutana 1/4/2010, imemsimamisha Uongozi Ndg. Salimu Mfungahema hadi itakapotangazwa vinginevyo kutokana na vitendo vyake vya kukosa uaminifu, maadili ya uongozi na matumizi mabaya ya madaraka aliyokuwa nayo. Uamuzi wa kutoa adhabu hiyo kwa kiongozi huyo, umetolewa baada vikao viwili tofauti kwa mujibu wa Kanuni za Maadili toleo la 2002 na Katiba ya CCM.

Awali, Bwana Mfungahema, alipewa muda wa zaidi ya mwenzi mmoja kujibu mambo mbalimbali yaliyokuwa yanamkabili au/na ili abadili mwenendo wake, lakini hakutekeleza

Pamoja na adhabu hiyo ,Kamati ya siasa imemweka chini ya uangalizi, na kwa kipindi chote anatakiwa asijihusishe na mambo yanayomhusu Katibu Mwenezi wa Tawi. Mambo yote yanayohusiana na Katibu Mwenezi wa Tawi yatafanya na Katibu wa Tawi hadi hapo itakapotangazwa vinginevyo. Ikigundulika anaendelea na siasa za chuki na kuwagawa wanachama , basi hatua nyingine kali zitachukuliwa dhidi yake.

Hata hivyo,Bwana Mfungahema bado ana haki yake ya kikatiba kukata rufaa dhidi ya hatua hiii ndani ya siku 15 tangu uamuzi huo ulipopitishwa rasmi, kama anadhani hajetendewa haki. Maelezo ya Rufaa yakiambatana na vielelezo yakinifu na ushahidi yanatakiwa yawasiliwe kwa katibu wa Tawi, na Baadae kujadiliwa na kamati husika kwa Mujibu wa Katiba ya Chama Cha Mapindizi ibara ya 19(2) Kushindwa kukata rufaa au Kamati kutoridhia vielelezo kutapelekea kuthibitishwa kwa adhabu dhidi yake.

Kutokana na sababu hizo, Kamati ya siasa imetumia madaraka yake iliyopewa kumsimamisha uongozi bila kumuonea kwa mujibu wa Katiba ya CCM Ibara ya ,39 (9) na mwongozo wa Tawi, na kanuni ya Maadili ya CCM..

Mwisho: kwa niaba ya Kamati ya siasa ya Tawi, Nawataka wanachama wote wa Tawi kudumisha umoja wetu kama kawaida na kufuatilia kwa karibu utendaji na taarifa za tawi ambazo zipo katika website ya Tawi www.ccmmoscow.blogspot.com ili kuondokana na Upotashaji wa Taarifa:. hasa kufahamu Taratibu za uchaguzi wa Viongozi wa Tawi letu hapa Urusi kwa kuanzia ngazi za mashina, Jumuiya ndani ya Tawi,na baadae Uchaguzi wa viongozi wa juu wa Tawi na wajumbe Kamati ya siasa , Mchakato huo wa Uchaguzi, ulijadiliwa na Kupitishwa na kikao cha Halmashauri kuu Tawi cha tarehe 27/3/2010. ambapo Utekelezaji wake Unaanza mapema zaidi 1 july 2010 kulingana na ratiba ya Mwongozo wa Uchaguzi Tawi la CCM MOSCOW:

Kidumu Cham cha Mapinduzi.

Aksanteni!

No comments:

Post a Comment