Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Friday, April 16, 2010

Kesi ya Mramba, Yona kuendelea jana!!!


Kutoka kulia ni Bw. Daniel Yona na Bw.Basil Mramba aliyekuwa Waziri wa Fedha.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, jana inatarajia kusikiliza kesi ya matumizi mabaya ya ofisi na kuisababishia serikali hasara ya Sh. bilioni 11.7, inayowakabili mawaziri wa zamani Basil Mramba, Daniel Yona na aliyekuwa Katibu Mkuu Gray Mgonja.

Kesi hiyo inatajarajiwa kutolewa uamuzi wa barua ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) iliyotolewa na shahidi wa tano, Ludovick Boniface wa upande wa mashtaka, ambapo upande wa utetezi walipinga kwa madai kuwa imeghushiwa.

Shahidi huyo ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Sekretarieti ya Bodi ya Sheria ya TRA Makao Makuu, alidai kuwa alitoa ushauri wa kisheria kutaka Kampuni ya Alex Sterwart (Assayers) Government Business Corporation isipewe msamaha wa kodi, lakini wizara ikapeleka barua kuishawishi TRA kutoa msamaha huo. Hata hivyo, upande wa mashitaka uliomba mahakama kupokea barua hiyo kama kielelezo, lakini upande wa utetezi ulipinga isipokelewe kwa madai kuwa imeghushiwa.

Katika kesi hiyo, washtakiwa wanadaiwa kuwa, kati ya Agosti mwaka 2002 na Juni 14, mwaka 2004, jijini Dar es Salaam, wakiwa watumishi wa umma kama mawaziri na katibu mkuu, walitumia vibaya madaraka. Ilidaiwa kuwa kwa kupitia kampuni ya Alex Stewart (ASSAYERS) ya Uingereza iliyoingia mkataba wa ukaguzi wa madini ambapo kwa kupitia kampuni tanzu ya Alex Stewart ( ASSAYERS) Government Business Corporation, waliingia mkataba kukagua kiwango cha uzalishaji wa madini ya dhahabu kinyume cha Sheria ya Manunuzi ya Umma.
Filed under: Uncategorized | 1 Comment

No comments:

Post a Comment