Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Monday, April 5, 2010

Kiongozi wa wazungu Afrika Kusini auwawa!!!


Eugene Terreblanche.

Kiongozi mwenye msimamo mkali wa wazungu nchini Afrika Kusini, Eugene Terreblanche, ameuwawa katika shamba lake kaskazini magharibi mwa nchi Polisi walisema Bw Terreblanche, ambaye alikuwa na umri wa miaka sitini na tisa, alipigwa na kukatwakatwa hadi kufa, katika kile kinacho-onekana kama mzozo juu ya mishahara ambayo haikulipwa.

Watu wawili wameshtakiwa kwa kuumwua kiongozi huyo.

Bw Terreblanche aliongoza chama cha wazungu wenye msimamo mkali cha AWB, ambacho kilishambulia kituo cha World Trade Centre mjini Johannesburg wakati mazungumzo yaliyolenga kumaliza utawala wa wazungu wachache yakiendelea.

Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, aliyataja mauaji ya kuongozi huyo kama kitendo kibaya, huku akitoa wito kwa raia kujituliza.

Zuma alisema raia wa Afrika Kusini kamwe wasikubali mtu yoyote kuitumia nafasi hii kuchochea uhasama kwa misingi ya rangi.

No comments:

Post a Comment