Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Tuesday, April 13, 2010

Madai Terreblanche alibaka yachunguzwa!


Polisi nchini Afrika ya Kusini wanapeleleza madai ya ubakaji kabla ya mauaji ya kiongozi wa siasa za ubaguzi wa rangi Eugene Terreblanche.
Wakili wa mmoja wa washtakiwa amesema Terreblanche alijaribu kufanya ngono na mmoja kati ya washtakiwa hao wawili.
Mwili wa Terreblanche ulikutwa kitandani ukiwa umevuliwa suruali.
Awali Polisi walisema mauaji hayo yalitokana na ubishi kuhusu mshahara, lakini sasa wanapeleleza uwezekano wa mauaji hayo yalitokana na kitendo cha kujitetea.
"Sisi hatutapeleleza kitu kimoja tu," alisema Musa Zondi wa kikosi maalum cha upelelezi wa makosa ya jinai nchini Afrika ya Kusini kinachoongoza uplelelezi wa kesi hiyo
Msemamji wa chama cha AWB ambacho Terreblanche alikuwa kiongozi wake amekanusha vikali madai ya ubakaji.

No comments:

Post a Comment