Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Friday, April 30, 2010

Vyandarua Vyageuzwa kuwa Net za Kuvulia Samaki!


Wakati Serikali na mashirika mbalimbali wakihangaika kugawa vyandarua kudhibiti ugonjwa wa malaria unaoua zaidi nchini, Wananchi wa Wilaya ya Babati mkoani Manyara wamebadili kazi ya vyandarua kuwa vifaa vya kuvulia samaki badala ya kujikinga na mbu.
Akielezea kisa hicho, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Mhe. Jesse Mlaki amesema jitihada kubwa zimefanyika kuleta maendeleo makubwa ya kukabili ugonjwa wa malaria wilayani humo, lakini cha kusikitisha baadhi ya wakazi wamehujumu juhudi hizo.

Amesema kuna mafanikio makubwa yanayotokana na elimu ya kujikinga na maambukizi ikiwa ni sambamba na ugawaji wa vifaa kama vyandarua ambapo familia nyingi zimepata vifaa hivyo.

Aidha mkurugenzi huyo amewataka wakazi wake kutambua hatari ya ugonjwa huo nchini na kujitahidi kuwakinga wanawake na watoto wachanga wanaogeuka wahanga wa ugonjwa huo kutokana na maambukizi ya mbu.

No comments:

Post a Comment