Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Saturday, April 10, 2010

Mawakili kuomba kumnusuru Babu Seya


MAWAKILI wa mwanamuziki maarufu nchini mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Nguza Viking, maarufu kama Babu Seya na mwanawe Johnson Nguza leo wanatarajia kuwasilisha maombi katika Mahakama ya Rufaa Tanzania yatakayoamua hatma ya mwisho ya wasanii hao.

Kiongozi wa mawakili hao, Mabere Marando, amesema, alisema kuwa walikuwa katika hatua za mwisho za kuandaa maombi kuiomba mahakama hiyo kupitia tena hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu dhidi wasanii hao waliohukumiwa kifungo cha maisha.

“Kanuni zinasema maombi yanaenda kwa majaji wale wale waliotoa hukumu ile, lakini Jaji Mkuu anao uwezo na mamlaka ya kuteua jopo jingine au kuongeza majaji zaidi katika jopo la awali kulingana na uzito wa kesi husika.” amesema Marando.

Amesema, kulingana na uzito wa kesi hiyo watamuomba Jaji Mkuu kuteua jopo lingine au kuongeza majaji zaidi kufanya mapitio katika hukumu ya awali iliyotolewa na Mahakama Kuu.

Mwaka 2004 Babu Seya na wanawe, Johnson Nguza maarufu kama Papii Kocha, Nguza Mbangu na Francis Nguza walihukumiwa kifungo cha maisha baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Kisutu, kuwatia hatiani kwa makosa ya kubaka na kuwalawiti watoto wa kike waliokuwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Mashujaa jijini Dar es Salaam.

Walikata rufaa ambayo Jaji Thomas Mihayo aliwatia hatiani na kuunga mkono hukumu ya Hakimu Mkazi Mkuu, Addy Lyamuya.

Katika hukumu ya Mahakama ya Rufaa iliyotolewa na jopo la majaji watatu, Salum Massati , Mbarouk Mbarouk, wakiongozwa na Jaji Nathalia Kimaro waliosikiliza rufaa hiyo iliyosomwa na Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufaa Neema Chusi.

Babu Seya na mwanawe Papii Kocha walitiwa hatiani, Nguza Mbangu na Francis Nguza wakiachiwa huru.

No comments:

Post a Comment